Kilwa kuwa bandari kubwa ya uvuvi Afrika Mashariki

HomeKitaifa

Kilwa kuwa bandari kubwa ya uvuvi Afrika Mashariki

Wilaya ya Kilwa iliyopo mkoani Lindi ni maarufu sana duniani kutokana na historia yake ya magofu ya kale na yenye vivutio vingi vya utalii.

Mji huo ambao unatajwa kuwa ndipo ustaarabu ulipoanzia, una bandari ya asili ambayo haina haja ya kuchimbwa kama inavyofanyika kwa bandari nyingine isipokuwa kwa kupenda au kwa sababu maalumu.

Kilwa ina bandari tayari lakini kutokana na kutumika sana kwenye uvuvi Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) sasa imeanza ujenzi wa gati kubwa litakalopokea meli kubwa za uvuvi za kimataifa. Bandari hiyo ya uvuvi itakuwa kubwa zaidi Afrika Mashariki.

Gati hilo linategemewa kuuchangamsha zaidi mji wa Kilwa kwenye uchumi, kuongeza ajira na meli zinazotia nanga hapo kuongezeka na bila shaka uchumi wa wilaya na mtu mmojammoja utaongezeka.

Uwepo wa bandari hiyo ya uvuvi itainua uzalishaji wa mazao ya uvuvi kwa wingi kutoka katika ukanda wa bahari tofauti na sasa ambapo mazao mengi yanayotumika yanatoka katika ukanda wa Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika.

error: Content is protected !!