LATRA yazikataa nauli za SGR

HomeKitaifa

LATRA yazikataa nauli za SGR

Mamlaka ya uthibiti wa usafiri wa ardhini nchini Tanzania (LATRA) yakanusha nauli zinazosambazwa mitandaoni zikitajwa kua ndio nauli zitakazotumika katika usafiri wa treni za umeme (SGR) nchini humo.

Kupitia vyanzo vyake vya Taarifa LATRA imedai kua, taarifa inayosambaza mitandaoni kuhusu nauli za SGR, sio rasmi na bado mchakato wa upatikanaji wa nauli muafaka katika usafiri wa treni ya umeme (SGR) unaendelea.

“..Tunapenda watanzania wafahamu kua LATRA haijatangaza nauli hizo, isipokua katika tangazo la mkutano wa wadau imenukuu nauli zilizopendekezwa na TRC, ili wadau, ikiwa ni pamoja na watumia huduma, Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini (LATRA CCC) na wananchi wote watoe maoni yao na kisha wataalamu wa LATRA wachambue hoja zote kisha waandae viwango vya nauli zitakazotumika na TRC kwa treni za abiria za SGR” wamesema latra katika taarifa yao iliyotolewa siku ya leo.

Hivi karibuni chapisho linaloonyesha orodha ya safari na nauli zitakazohusika katika usafiri wa treni ya umeme (SGR) nchini Tanzania lilisambaa mitandaoni huku likionesha viwango vikubwa vya nauli kuliko yalivyokuwa matarajio ya wengi na kuzua mijadala miongoni mwa Watanzania juu ya nauli hizo na wengine kuanza kuitupia lawama LATRA na Serikali kwa ujumla.

error: Content is protected !!