Maagizo ya Rais Samia kusaidia machinga.

HomeKitaifa

Maagizo ya Rais Samia kusaidia machinga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa watumishi wa kada mbalimbali serikalini kwa ajili ya kusaidia kuboresha mazingira ya wafanya biashara wadogo wadogo maarufu kama machinga.

Akizungumza leo hii alipokutana viongozi wa machinga jijini Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu alitoa maagizo mbalimbali ikiwemo yafuatayo:Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini “LATRA”, imetakiwa kufungua njia mbalimbali kusaidia wateja kufikia maeneo ambayo machinga wamehamia na hakuna njia za kuwezesha wateja kufika.

Rais Samia amesema maendeleo ni kwenda pamoja hivyo wanatakiwa wakae na kuangalia sheria  na kanuni ili waweze kuruhusu daladala kwenda maeneo ambayo machinga wapo.Kuwa na vitambulisho vilivyoboreshwa.

Rais Samia amesema machinga sasa wameamua kutambulika kama kundi maalum na hivyo wanatakiwa kuwa na vitambulisho vilivyoboreshwa ambavyo vitakua vya kudumu tofauti na vya sasa. Vitambulisho ambavyo serikali inaazimia kuvitoa kwa machinga ni vile ambazo vikiingaliwa kwenye mtandao vinaweza kutoa taarifa zote kuhusu machinga. Ulipaji wa kodi kulingana na uwezo wa biashara.

Machinga wametakiwa kulipa kodi ili kusaidia serikali kuendelea kuboresha mazingira yao kwa kuwajengea masoko ya kisasa. Rais Samia amesema kwa sasa wamachinga wanatumia kodi za wengine kutengenezewa mazingira yao hivyo watakapokua wamekaa sawa wanatakiwa waanze kulipa kodi kwa serikali.Pamoja na hayo Rais Samia amesema Serikali imeongea na mabenki kwaajili ya kuwapatia mikopo machinga lakini pia alibainisha kuwa serikali inajenga soko la Kariakoo ambalo liliungua na baadae watajenga soko jipya maeneo ya Jangwani ambalo litaweza kubeba wafanyabiashara zaidi ya 4,000.

error: Content is protected !!