Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wa uchaguzi unaotumika na Tume hiyo umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na chama cha siasa, hususan Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na madai kwamba zoezi la upigaji kura tayari limefanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa INEC, Ramadhan Kailima kupitia taarifa ya INEC ya Agosti 23, 2025, amesema taarifa hizo zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni za uongo na upotoshaji zenye lengo la kupotosha umma na kuibua taharuki.
View this post on Instagram