Mahakama yaja na teknolojia ya akili bandia

HomeKitaifa

Mahakama yaja na teknolojia ya akili bandia

Akizungumzia kuhusu wiki ya siku ya sheria na siku ya Sheria, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa, ili kuhakikisha mhimili  wa Mahakama unaendana na mapinduzi ya nne ya viwanda duniani unatarajia  kuanza kutumia akili bandia kwenye utoaji huduma na haki.

Prof Juma alisema Tanzania inajifunza zaidi kupitia India ambako teknolojia ya akili bandia ilitengenezwa, teknolojia hiyo ina uwezo wa kutafsiri zaidi ya lugha tisa zinazozungumzwa katika ukanda wa bara la Hindi. Na kusema kuwa utumiaji wa teknolojia hiyo haimaanishi kuwa itachukua kazi za majaji na mahakimu.

“Akili bandia si kujua lugha nyingi tu, bali ni kutengeneza mashine inayoweza kufanya kazi kama binadamu. Mambo yanayoweza kufanywa na akili bandia hivi sasa ni kuelewa lugha ya binadamu na kwa sasa ni kuelewa lugha ya binadamu na kwa sasa tunakusanya sauti kwa wenzetu wa wa TBC na Zanzibar, ili mfumo huu uweze kujifunza” alisema Profesa Juma.

Pamoja na hayo ili kuhakikisha mfumo wa akili bandia unajifunza kiswahili na msamiati wake wa mahakamani, tangu Desemba 23 mwaka jana majaji mahakimu na wafawidhi wake wa mahakamani  wa mahakamani wanarekodi mashauri yote yasiozidi saa moja.

error: Content is protected !!