Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 7.79 katika kipindi cha mwezi Julai – Septemba sawa na ufanisi wa asilimia 104.9 wa lengo la kukusanya shilingi trilioni 7.42.
Taarifa kutoka TRA imesema hiki ni kiwango cha juu kabisa ambacho hakijawahi kufikiwa na TRA kwa mwezi Julai – Septemba ya mwaka wa fedha.
#kodi
Rekodi mpya ya makusanyo imeandikwa. pic.twitter.com/kmkVVya9QJ— TRA Tanzania (@TRATanzania) October 1, 2024
Sababu ya ongezeko hilo
TRA imetaja sababu za kuwa na ongezeko hilo ni pamoja na;
1. Kuendelea kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya Rais Samia Suluhu ya kuendelea kuhamasisha ulipaji kodi
2. Kukua kwa ushirikiano na mahusiano kati ya TRA na walipa kodi
3. Kuendelea kuweka kipaumbele utoaji wa huduma bora kwa walipakodi
4. Ongezeko la matumizi ya TEHAMA katika ukusanyaji kodi
5. Kufuatilia na kuchukua hatua za haraka za kutatua changamoto