Mambo 5 muhimu ya kufanya asubuhi yatakayofanya siku yako kuwa bora

HomeElimu

Mambo 5 muhimu ya kufanya asubuhi yatakayofanya siku yako kuwa bora

Siku yako kuwa nzuri au mbaya inategemea jinsi unavyoianza. Kuna mambo ambayo ukiyafanya asubuhi yanaweza kuifanya siku yako kuwa bora au kuwa mbaya. Soma hapa ni mambo 5 ya kufanya asubuhi yatakayopelekea siku yako kuwa bora sana.

Fanya sala au maombi
Mara tu uamkapo kulingana na imani yako, fanya sala ili kujiunganisha na chanzo chako cha kiroho, ili kukuongoza kwenye siku yako. Usiruhusu kuanza siku yako bila kupata muda wa kufanya sala, fanya sala yako angalau kwa dakika 5.Unaweza pia kufanya tajuhudi (meditation). Kuna aina nyingi za tajuhudi lakini mara nyingi tajuhudi ni kitendo cha kuvuta pumzi ndani na kuitoa nje baada ya muda.Kumekuwa na shuhuda nyingi kuhusu faida za kufanya tajuhudi kwa watu ambao wamekuwa wanafanya tajuhudi mara kwa mara. Faida za tajuhudi ni kama kupunguza msongo wa mawazo (stress), kuondoa hofu, kupona magonjwa, kuongeza ufanisi na kukua kiroho.

Anza na maneno chanya
Hakikisha unaianza siku yako kwa kuongea au kuandika maneno ya hamasa. Maneno kama mimi ni bora, naweza, Mungu siku zote yuko pamoja nami, mimi ni mshindi, naenda kufanya kilicho bora na nategemea kupata kilicho bora, leo ni siku yangu n.k. Maneno haya yakufanya umiliki na uanze siku yako kwa hamasa na ubora wa hali juu. Hii itakufanya uwe na siku bora.

Fanya mazoezi
Kufanya mazoezi kutafanya uanze siku yako kwa hamasa huku mwili wako ukiwa na nguvu. Kufanya mzoezi kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuepuka magonjwa kama ya kisukari na magojwa ya moyo. Hasa kwa ulimwengu wetu huu wa sasa ambao kazi nyingi tunafanya tukiwa tumekaa, mazoezi ni jambo la muhimu sana. Unaweza kupiga mazoezi sambamba na kusikiliza nyimbo za hamasa, hii itakufanya upate hamasa ya kufanya mazoezi hata kipindi ambacho ujisikii kufanya mazoezi.

> Mambo 10 muhimu ya kufanya asubuhi siku yako iwe nzuri

Soma kitabu
Asubuhi ni muda mzuri wa kusoma kitabu, kabla ya kufanya majukumu mengine. Kama una shughuli nyingi na unakosa muda wa kusoma kitabu, asubuhi ni muda mzuri sana. Unaweza kusoma kurasa 5 mpaka 10 kila siku asubuhi. Kama unasoma kurusa kumi, kwa kitabu cha kawaida itakuchukua muda mfupi kumaliza kitabu kimoja. Hii ni hatua kubwa utakuwa umepiga mbali na kujenga tabia ya kusoma vitabu utakuwa umejifunza mengi sana yatakayokusaidia kwenye safari yako ya mafanikio.

Panga ratiba yako ya siku
Jambo la mwisho na muhimu kabisa ni kupangilia ratiba yako ya siku. Kabla ujaanza kufanya majukumu ya siku hakikisha unakuwa na ratiba nzima ya siku yako. Hakikisha unajua kwenye siku yako unaenda kufanya nini na kwa muda gani. Hii itakusaidia kukwepa vitu ambavyo vinakuibia muda wako kama kupiga soga, kufatilia mitandao ya kijamii na habari ambazo hazikuhusu, lakini pia itakusaidia kutumia muda wako vizuri kwa kufanya yale ambayo ni muhimu sana kwako.

Kupitia mambo hayo 5 unayoweza kufanya asubuhi ambayo yatapelekea uwe na siku bora. Ianze siku yako kwa kufanya mambo haya na, ni ahadi yangu kwako, maisha yako hayatabaki kuwa kuwa ya kawaida.

error: Content is protected !!