Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki uzinduzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Mboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayoiagiza Serikali kuhakikisha wakulima wananufaika sekta ya kilimo.
Ushiriki wake katika mkutano huo unatoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kujifunza njia bora za kufanya kilimo pamoja na matumizi ya teknolojia.
Akihutubia katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula- AGRF 2023, Rais Samia alisema weka wazi nia ya Serikali ya kutumia TEHAMA kwenye shughuli za kilimo.
“Matumizi ya TEHAMA hayaepukiki kwenye kilimo na Serikali imejipanga kuendana na kasi ya mapinduzi hayo ya kilimo,” alisema Rais Samia.
Sekta ya mboga na matunda imeonekana kuwa na umuhimu na hivyo kwa kushiriki katika mkutano huu wakulima watapa kujifunza njia bora za kuongeza thamani ya mazao yao ili yaweze kuuzika katika masoko makubwa duniani.