Marais wa nchi tofauti kuhudhuria sherehe za uhuru

HomeKitaifa

Marais wa nchi tofauti kuhudhuria sherehe za uhuru

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema Marais wa nchi tano wamethibitisha kuhudhuria sherehe za miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara leo kwenye uwanja wa Uhuru  jijini Dar es Salaam.

Marais waliothibitisha kuwa watakuwepo ni Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Azali Assoumani wa Visiwa vya Comoro, Filipe Nyusi wa msumbiji na Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Wizara hiyo pia imesema Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombaza atamuwakilisha Rais wa nchi hiyo, Evariste Ndayishimiye, Naibu Waziri Mkuu wa Eswatini, Themba Masuku atamuwakilisha Mfalme Muswati.

Aidha, imeeleza kuwa Rais mstaafu wa Malawi, Dk. Joyce Banda atamuwakilisha Rais wa nchi hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Lazarus Chakwera.

error: Content is protected !!