Mashabiki wa Arsenal wakamatwa

HomeKimataifa

Mashabiki wa Arsenal wakamatwa

Polisi nchini Uganda imewakamata mashabiki 20 wanaoshangilia timu ya Arsenal baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Manchester United katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Emirates.

Mashabiki hao walikamatwa jana Januari 22, 2023 baada ya ushindi dhidi ya Manchester wakipiga gwaride la kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu England katika Jiji la Jinja nchini humo.

“Sijui tumefanya nini lakini tulikuwa tukisherehekea ushindi wetu dhidi ya wapinzani wetu Manchester United,” alisema mmoja wa mashabiki hao, Kasule na kuongeza kuwa “ni wafuasi 20 kwa jumla tuliokamatwa katika Jiji la Jinja.”

Mmoja wa maofisa wa polisi kituo cha Jinja, Maurice Niyonzima aliulizwa sababu za kuwashikilia mashabiki hao na kusema kituo hicho kina msemaji wake.

error: Content is protected !!