Dawa ya usafirishaji binadamu yapatikana

HomeKitaifa

Dawa ya usafirishaji binadamu yapatikana

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera, Bunge, Ajira , kazi, vijana na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema katika kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu, serikali imesema kuwa itapeleka wafanyakazi wa majumbani katika nchi ambazo imeingia nazo mkataba na si vinginevyo.

“Hivi sasa tumetengeneza mwongozo mpya ambao utawabana mawakala wa huduma za ajira na tutahakikisha kuwa tutasafirisha tu wafanyakazi katika nchi zile ambazo tumeingia nazo mkataba na siyo vinginevyo”.

Mwanzo serikali ilipiga marufuku utaratibu wa mawakala wa kampuni za ajira kusafirisha wafanyakazi wa majumbani, kutokana na kuwepo kwa makubaliano ya kwenda kufanya kazi za ndani lakini wakifika wanafanyishwa kazi tofauti na ambazo walikubaliana.

“Mwaka 2018 nilipiga marufuku usafirishaji wa wafanyakazi hawa kama kuna mtu ambaye amekwenda katika kipindi hiki baada ya mimi kupiga marufuku, Basi huyo amekwenda kinyume na utaratribu hivi sasa tumeingia mkataba na Qatar ambayo ndiyo tutawapeleka wafanyakazi”.

error: Content is protected !!