Waliorusha picha za ajali Mtwara wasakwa

HomeKitaifa

Waliorusha picha za ajali Mtwara wasakwa

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka mara moja wale wote waliosambaza picha za miili ya watoto wa shule ya msingi King David waliofariki katika ajali Julai 26, 2022 kujisalimisha.

“MwanaMtwara, Mtanzania aliyerusha picha zile kwenye mitandao ya kijamii asubuhi ya leo, hiyo ni tabia isiyokuwa ya kiungwana na nimtake aliyerusha picha zile yeye mwenye tu ajitokeze na ni muhimu akaomba msamaha kwa Wanamtwara na watanzania,” alisema Brigedia Marco Gaguti. 

Naye Father Patrick Mwaya kutoka Kanisa la Roman Catholic Mtwara amelaani kitendo hicho cha kurusha picha za miili ya watoto hao katika mitandao ya kijamii.

“Kwa upande wa msimo wa kanisa niseme wazi ni aibu, ni marufuku na ni fedhea kuweka picha za marehemu kwenye mtandao na kuzionyesha waziwazi,” alisema Father Mwaya. 

Vifo vyao vinafanya idadi ya vifo kufikia Watu 13 huku wawili kati yao wakiwa ni Dereva na Mwangalizi mmoja wa Wanafunzi ambapo miili ya Wanafunzi hao imeagwa leo katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula.

error: Content is protected !!