Mbuzi na Kondoo wapatwa na kizunguzungu

HomeKitaifa

Mbuzi na Kondoo wapatwa na kizunguzungu

Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimetoa taarifa ya matokeo ya Utafiti wa ugonjwa wa kizunguzungu kwa mbuzi na kondoo.

Utafiti huo uliofadhiliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)  umefanywa katika halmashauri ya wilaya ya babati Ikihusisha wafugaji wa mbuzi na kondoo wa wilaya hiyo.

“Ugonjwa wa kizunguzungu kwa mbuzi na kondoo ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo Tegu wakubwa aina ya Taenia multiceps ambao hukaa kwenye utumbo mwembamba wa mbwa ambako hutaga mayai na kutoka kupitia kinyesi chake Mpaka kwenye mazingira yaani udongo, maji na majani,” alisema Dkt. Jahashi Nzalawahe.

Dkt. Nzalawahe ambaye ni mtafiti wa ugonjwa huo kutoka SUA alisema mayai hayo hukaa kwenye mazingira tajwa kwa muda mrefu ambapo mbuzi na kondoo huambukizwa kwa Njia ya kula majani na kunywa maji.

Alisema ugonjwa huo ukiwapata mbuzi na kondoo huwa hawaponi.

Akizungumza kwa niaba ya wafugaji, Dorcas alisema wamekuwa wakipata hasara ya Mifugo kufa pasipokujua nini tatizo lakini baada ya kupata elimu hiyo imewasaidia kupunguza vifo.

Mkutano huo umefunguliwa  na Adam Ipingika diwani kata ya kisangaji tarehe 20 Julai, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

 

error: Content is protected !!