Mhudumu wa afya aliyemshona mgonjwa na kumfumua makusudi apatikana

HomeUncategorized

Mhudumu wa afya aliyemshona mgonjwa na kumfumua makusudi apatikana

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imefanikiwa kumpata mhudumu wa afya ambaye video yake imesambaa baada ya kumfumua mgonjwa nyuzi  kwenye kidonda chake kisa ameshindwa kulipia gharama za matibabu.

TAMISEMI imesema “tukio hili ni la July 2021 na mtumishi huyu aliyekiuka miiko ya udaktari anaitwa Jackson Meli, ni Clinical Officer wa Kituo cha Afya Kerenge Tarafa ya Magoma, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.”

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ameshachukua hatua kwa kumsimamisha kazi na amempa hati ya mashtaka na pia ameshafikishwa kwenye Baraza la Taaluma ili achukuliwe hatua stahiki kwa kwenda kinyume na miiko ya taaluma ya udaktari.

error: Content is protected !!