Van Damme balozi wa DRC

HomeBurudani

Van Damme balozi wa DRC

Mwigizaji nyota wa zamani raia wa Ureno, Jean-Claude Van Damme (61) amepewa heshima ya kuitangaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) na kuahidi kuwashawishi waigizaji wengine nyota wa zamanikuungana naye katika jukumu hilo akiwamo Arnold Schwarzenegger.

“Nitajaribu kuwasahwishi nyota wa kimataifa katika tasnia mbalimbali za uigizaji lakini pamoja na wanamuziki maarufu kama Jennifer Lopez na wanasoka maarufu duniani kama Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Ronaldinho.

“DRC ina utajiri wa madini wa Dola trilioni 36, hivyo kazi yangu ni kutafuta wawekezaji wanaolewa hilo na wako tayari kutoa kwanza kabla ya kuanza kupokea na watakaokuwa na imani na Rais Felix Tshisekedi,” alisema Van Damme.

Uteuzi wa Van Damme kuwa Balozi DRC katika jumuiya ya kimataifa unalenga kuueleza ulimwengu ukweli kuhusu rasilimali za DRC, kutangaza vivutio, utamaduni na amani ya taifa.

 

error: Content is protected !!