Mtangazaji wa redio na televisheni kutoka nchini Tanzania, Meena Ally amekanusha kuhusu video ya utupu inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kumuonyesha mtu anayefanana na yeye iliyofanya watu waamini kwamba ni yeye.
Kwenye tamko hilo Meena ameanza kwa kutoa pole kwa familia yake, mashabiki, wafanyakazi wenzake na wadau wake kutokana na kadhia hiyo na kusisitiza kwamba msichana anayeonekana pale sio yeye na wala hausiki wana watu waliosambaza video hiyo.
“Ninaandika haya kwa sababu si tu nafananishwa na msichana alie katika video hiyo, bali pia kuna mahali kwenye video hiyo imeandikwa jina langu”
“Nawasihi Watanzania wenzangu wasihusike katika kuisambaza hii video zaidi kwani tayari nimeshaifungulia kesi na upelelezi unaendelea kumtafuta aliyeisambaza na kuihusisha na jina langu na kampuni ninayofanya kazi Cloudsfmtz” ameandika Meena.
Watu wengi mashuhuri pamoja na mashabiki wa Meena wamekemea vikali kitendo kama hichi cha udhalilishaji wa mtandaoni kwani ni kinyume na sheria za nchi na utu wa binadamu, baadhi ya watu hao ni mtangazaji Millardayo, mwanamuziki Shetta, Flaviana Matata, Salama Jabir, Frida Amani na Mayunga.