Kwenye uchaguzi wa Guinea mwaka 2010, Alpha Conde alikuwa mpinzani mkuu kwa Serikali iliyokuwa ikimaliza muda wake. Alipendwa na wanaharakati wa masuala ya demokrasia na haki za binadamu kwa ujumla.
Alpha Conde aliyezaliwa Machi 4 1938, alikuwa mpinzani wa Serikali tangu enzi za Rais wa kwanza wa Taifa hilo, Ahmed Sekou Toure. Alileta upinzani mkubwa kwa Rais wa zamani Lansana Conte ambaye alichuana naye vikali kwenye mbio za Urais mwaka 1993 na mwaka 1998.
Saa kadhaa kabla ya uchaguzi wa mwaka 1998, Conde alikamatwa akituhumiwa kutaka kuipindua Serikali na akafungwa kwa miaka miwili.
Mwaka 2010, Conte aliingia kwenye historia ya Guinea kwa kuwa Rais wa kwanza aliyechaguliwa kwenye uchaguzi huru. Kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa, Conde alisema “Nitajitahidi kuwa ‘Mandela wa Guinea’, nitawaunganisha wana wote wa Guinea”
Kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, alishinda Urais kwa kupata 58% ya kura. 2020% alishinda tena kwa kupa 59.8% ya kura na hapo zikaibuka tuhuma kwamba ‘amechakachua’.
Na sasa anepinduliwa na jeshi, huku Umoja wa Afrika ukipinga vikali mapinduzi hayo.