Miche ya tende kuzalishwa nchini kupanua kilimo cha zao hilo

HomeBiashara

Miche ya tende kuzalishwa nchini kupanua kilimo cha zao hilo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Profesa Peter Msofe amesema serikali imeanza utafiti wa kuzalisha miche kwaajili ya kuendeleza zao la Tende kwa lengo la kuongeza upatikanaji wake kirahisi nchini.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya wafanyabiashara waliojitokeza kwenye Maadhimisho ya 46 ya Siku ya Chakula Duniani  yanayofanyika kitaifa Mkoani Tanga Profesa Msofe amesema kuwa utafiti huo ukikamilika utasaidia kuongeza uzalishaji wa zao la Tende nchini.

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania,(TARI) Gasper Mgimiloko amesema mpaka sasa wanazo mbegu zaidi ya 3700 ambazo zinafanyiwa utafiti na kuzalishwa na zikikamilika zitasambazwa kwa wananchi.

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania,(TARI)  Joseph Nzunda amesema  tayari wameshatambua mikoa ambayo itafanyiwa majaribio ya mbegu hizo kutokana na hali ya hewa ya maeneo hayo.

 

error: Content is protected !!