Mikoa 3 inayoongoza kwa kelele

HomeKitaifa

Mikoa 3 inayoongoza kwa kelele

Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) imetaja mikoa mitatu inayoongoza kwa malalamiko ya kelele kuwa ni Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma na kubainisha kuwa nyumba za ibada na maeneo ya starehe yanaongoza kwa kulalamikiwa kuwa na makelele.

Taarifa hiyo imetolewa na Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria na Ufuatiliaji kutoka NEMC, Ndimbuni Mboneke wakati akizungumza kwenye warsha ya Maofisa Mazingira wa Mikoa na Wilaya.

“Siku za hivi karibuni kumekuwapo na shida sana ya kelele kutoka kwenye maeneo mbalimbali nyumba za ibada,kumbi za starehe na kukua kwa teknolojia, kuongezeka kwa idadi ya watu na shughuli za kibinadamu,

“Kelele zinasababisha watu washindwe kulala na akishindwa kulala anashindwa kufanya kazi zake za siku kwa sababu anakuwa hajapata usingizi vizuri,” alisema Meneja Mboneke.

Aidha, Meneja Mboneke amewataka watoa leseni kuhakikisha wanasimamia vyema sheria na taratibu zilizowekwa na pia kuchukua hatua pale zinapokiukwa.

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!