Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ametangaza kuachia nafasi ya uenyekiti katika bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo.
Mo amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kikao kilichofanyika Septemba 21, 2021 yeye kuachia ngazi na kutokana na kutokuwepo nchini mara nyingi kwa sababu ya kuwa na safari nyingi kikazi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo ameweka video inayoonesha akitoa ufafanuzi juu ya sababu zilizosababisha bodi kufikia uamuzi huo.
Ameeleza zaidi kwamba uwepo wa mwenyekiti wa bodi ni muhimu sana, hivyo kutokana na yeye kusafiri muda mwingi anakuwa hayupo nchini, hivyo imemlazimu kuachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine.
“Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Wana-simba, mmetuunga mkono katika kipindi changu cha uongozi cha miaka minne, kwani bila ninyi tusingeweza kufika hapa, pia ninawashukuru viongozi wote wa Simba na wajumbe wa bodi kwa kunipa ushirikiano kwenye uongozi wangu,” amesema.
Mo amemteua makamu wake, Salim Abdallah, maarufu “Try again” kuchukua nafasi hiyo uewenyekiti wa bodi ya Simba, na amesema kuwa ana uzoefu mkubwa kwenye uongozi wa klabu hiyo na walishirikiana vizuri kuijenga Simba kipindi cha uongozi wake.
View this post on Instagram