Mourinho avuna mkwanja mrefu kwa kufutwa kazi

HomeMichezo

Mourinho avuna mkwanja mrefu kwa kufutwa kazi

Kufukuzwa kazi kunaweza kukawa ni kilio kwa mwingine, lakini kwake Jose Mourinho ‘The Specila One’ ni furaha, nderemo na vifijo. Inaripotiwa kuwa Mourinho kufukuzwa kwake katika mara nne katika vilabu vitatu vya Chelsea, Manchester United, Tottenham nchini Uingereza kumeingizia takribani shilingi bilioni 200.

Kazi yake ya kwanza kabisa katika Ligi Kuu England Mourinho alianza kukinoa kikosi cha darajani, Chelsea mnamo 2004 na kufanikiwa kuchukua Kombe la Ligi Kuu England mara mbili mfululizo. Lakini mwaka 2007 Mourinho akafungashiwa virago na Roman Abramovich baada ya kuwa na mgogoro baina yao ambao haujawekwa bayana hadi leo.

Miaka sita baadae Mourinho akarudi tena darajani, kama kawaida yake akaiwezesha Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mwaka 2015 na muda haukukawia mambo yakaanza kwenda kombo baada ya mfululizo wa matokea mabaya ya Chelsea, Abramovich uzalendo ukamshinda akamfungashia virago Mourinho kwa mara ya pili.

Haikuchukua muda Mourinho kurejea tana katika nchi ya Malkia, msimu wa majira ya joto Manchester United wakampa kandarasi ya kuiona klabu yao. Msimu wake wa kwanza Mourinho akanyanyua ndoo ya Europa League na Manchester United kushika nafasi ya pili ya msimamo Ligi Kuu England. Msimu wa tatu tamu ikawa chungu, matokeo mabovu ya Manchester United yakamfanya Mourinho asiwe Manchester wakati wa Christmas 2018, akatimuliwa tena.

Mwaka uliofuata Tottenham wakataka huduma yake. Unaambiwa katika maisha ya ukocha ya Mourinho hakuna wakati Mourinho amekuwa na wakati mbaya kama wakati anaifundisha Tottenham, kwani hakushinda kikombe chochote, hii si kama ilivyo ada yake. Tottenham wakaona isiwe tabu, wakavunja kandarasi na kumfukuza.

Kufukuzwa kwa Mourinho mara nne katika vilabu vitatu Ligi Kuu England, kumeingizia bilioni 200 kama fidia za mikataba yake. Huu ni utafiti uliofanywa na 101 Great Goals.

error: Content is protected !!