Kibarua cha Solskjaer Manchester matatani

HomeMichezo

Kibarua cha Solskjaer Manchester matatani

Klabu ya Manchester United imepoteza michezo mitatu katika michezo yao minne ya mwisho. Baada ya mpira wa adhabu (pentali) ya mchezaji wao Bruno Fernandes kuota mbawa mwisho wa juma lililopita na Manchester kupoteza mchezo huo kwa bao moja kwa sifuri, kibarua cha kocha Solskjaer kimekuwa matatani sana.

Usiku wa leo Manchester United itakutana na Klabu ya Villarreal ya Uhispani kwenye hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Ulaya. Mchezo huu unaongeza shinikizo kwenye kibarua cha Soskjaer kwani tayari amepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya klabu ya Young Boys.

Tabu inaongezeka upande wa kocha huyo kwakuwa taaba ya mchezo wa Klabu bingwa dhidi ya Villarreal, atabaliana na ratiba ngumu ya Ligi Kuu England ambapo atacheza na Everton, Liverpool, Tottenham na Manchester City kwenye michezo inayofuata.

Vyombo vya habari vya ndani ya Uingereza vinasema kuwa huenda kibarua chake kikaota nyasi kama ataendelea kuwa na muendelezo wa matokeo mabaya.

error: Content is protected !!