Ajira rasmi 10 zinazolipa zaidi nchini Tanzania

HomeElimu

Ajira rasmi 10 zinazolipa zaidi nchini Tanzania

Ajira ni moja ya njia ya kujiingizia kipato. Lakini ukweli ni kwamba kila ajira ina ujira wake, hii ni kulingana na mazingira ya kazi, elimu na hata uzoefu. Kwa mwaka 2021, Clickhabari imekukusanyia idadi ya ajira 10 zinazolipa zaidi Tanzania.

Muhimu: Orodha hii haijafuata mtitiriko wa ajira inayolipa zaidi kwenda ya mwisho, au kinyume chake.

Urubani
Hii ni moja ya kazi adimu sana Tanzania, pia ni kazi ambayo kwa Tanzania ndio inalipa sana na yenye marupurupu. Mshahara wa rubani anayeanza kazi haunza kwa Sh. 902,000/- hadi 2,950,000/- ukichanganya na marupurupu.

Sheria
Kwanza ni moja ya kazi inayoheshimika sana Tanzania. Kwenye Sheria unaweza kufanya kazi kama mshauri wa masuala ya kisheria, wakili, hakimu au hata Jaji. Kwa Tanzania unaweza kuwa mwanasheria unayejitegemea, Mwanasheria wa Serikali, asasi ya kiraia au hata kampuni. Mwanasheria anaweza kupata mshahara kati ya milioni 1,530,000/- shilingi hadi 5,010,000/-3.

Utabibu/Udaktari
Hii moja ya kazi pendwa na pia zinazoheshimika kwa kiasi kikubwa sana Tanzania. Fani hii husomewa kwa miaka isiyopungua mitano hadi kuhitimu shahada yake. Mtu ana hiari ya kufanya kazi hii serikalini au katika taasisi binafsi. Madaktari hupokea mshahara kati ya Shilingi 2,250,000/- mpaka 7,370,000/- kwa mwezi.

Uhandisi
Uhandisi uko wa namna tofauti, kuna wa vifaa vya umeme, magari, barabara, majengo na kadhalika. Katika hizi, haijalishi unapendelea kufanya ipi, lakini kila moja ina ujira mzuri tu. Mathalani, ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania umetoa fursa nyingi sana kwa wahandisi kwa kada zote. Wahandisi Tanzania wanakadiriwa kupokea kiasi kati ya shilingi 1,350,000 hadi 4,420,000/- kwa mwezi.

Uandishi wa Habari
Ni moja ya kazi zinazolipa vizuri kama utapata bahati ya kufanya kazi katika kituo kikubwa cha Habari. Katika tasnia hii mtu anaweza kufanya kazi kwenye gazeti, televisheni au hata radio. Kwa mfano, katika gazeti la Citizen, mshahara wa mwandishi ni shilingi 1,200,000 kwa mwezi.

Uhasibu
Sekta ya fedha ni moja ya sehemu ambayo mtu anaweza kupata mshahara mzuri. Wahasibu ambao hulipwa mshahara mzuri mara nyingi ni wale wenye CPA, hawa hulipwa misharaha kati ya 1,500,000 hadi 2,500,000/- kwa mwezi.

Uhadhiri
Hii pia ni moja ya kazi zinazolipa vizuri Tanzania. Malipo hupanda zaidi kulingana na uzoefu kazini na kiwango cha elimu. Wahadhiri kwenye vyuo maarufu na vikubwa zaidi hulipwa fedha nzuri kati ya shilingi 1,080,000/- hadi shilingi 3,540,000/- kwa mwezi.

TEHAMA
Tasnia hii ni tasnia mtambuka. Inahusisha kutengeneza tovuti, programu tumishi kwa ajili ya kazi fulani na masuala yote ya mawasiliano ya mitandao. Kama ikitokea kupata kazi katika sehemu nzuri kama kampuni za kimataifa, basi mshahara unaweza ukawa mzuri zaidi. Mshahara unaweza ukawa kati ya shilingi 812,000 hadi 2,650,000.

Afisa Masoko
Kazi hii inaweza kukupa kipato kizuri sana kama mtu atapata nafasi ya kufanya kazi katika taasisi kubwa. Afisa masoko ana kazi kubwa sana kuhakikisha bidhaa au huduma ya taasisi inakwenda vyema na mauzo kuongezeka. Katika viwanda vikubwa afisa masoko anaweza kulipwa kati ya shilingi 1,200,000 hadi 2,000,000.

Upishi
Ni moja ya kazi ambayo kama mtu atapata kazi hii katika mgahawa au hoteli kubwa nchini Tanzania, basi anaweza kulipwa fedha nzuri sana. Kazi hii hutegemea uzoefu mara nyingine, au hata aina ya ujuzi wa mapishi au hata uwezo wa kupika vyakula kulingana na mila na desturi za watu wengine duniani. Lakini kazi hii sio lazima mtu aajiriwe mara nyingine, bali unaweza kupata tenda kwenye shughuli mbalimbali kama harusi, misiba na kadhalika na ukapata fedha nzuri tu. Kwa waajiriwa, huweza kulipwa kati ya Sh. 1,000,000/- hadi 1,500,000/- kwa mwezi.

error: Content is protected !!