Dereva aeleza alichomwambia Ole Nasha kabla hajafariki

HomeKitaifa

Dereva aeleza alichomwambia Ole Nasha kabla hajafariki

Fikiri Madinda, dereva  wa aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, William Tate Ole Nasha ambaye alifariki Dunia Septemba 27 mwaka huu jijini Dodoma amefunguka na kusema kuwa marehemu alikua mzima wa afya kabla mauti kumkuta.

Ameeleza zaidi na kusema alipokwenda kumchukua hotelini, alimweleza kuwa usiku wake alikuwa akisumbuliwa na presha, lakini kwa kuwa alirudi katika hali ya awali, hivyo waanze safari.

“Tangu tutoke Arusha hakuwa na tatzio lolote, hata tulipokuwa njiani hadi tunafika anapoishi katika eneo la Medeli, niliagana naye na kumweleza nitamtafuta saa tatu kwa ajili ya kumpeleka kwenye utekelezaji wa majukumu yake,” amesema.

> Hapa ndipo atakapozikwa Marehemu Ole Nasha

Kifo cha Waziri Ole Nasha ni pigo kwa nchi yetu kama alivyoeleza Rais Samia kwamba taifa limepoteza mtumishi mchapakazi na mwaminifu wa serikali.

Katika ujumbe wake, Rais Samia alisema “Nasikitika kuwajulisha kuwa aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Mhe. William Tate Ole Nasha amefariki dunia Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Spika Mhe. Job Ndugai, Wabunge, Familia na Wananchi wa Ngorongoro. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”

error: Content is protected !!