14 wakamatwa kwa tuhuma za kupora katika ajali Tanga

HomeKitaifa

14 wakamatwa kwa tuhuma za kupora katika ajali Tanga

Jeshi la Polisi, Mkoa wa Tanga limewakamata watu 14 ambao wanatuhumiwa kufanya uporaji katika ajali iliyohusisha vifo vya watu 20 na majeruhi 12 iliyotokea hivi karibuni wilayani Korogwe.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Tanga, Henry Mwaibambe alisema watu hao walikamatwa kupitia msako huo wa polisi.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa na baadhi ya vitu ambavyo baada ya kuwahoji ilibainika kuwa walivipata kutokana na kuiba wakati wa ajali hiyo.

“Tutashirikiana na ndugu wa familia kubaini mali zao ambazo ziliibwa siku ya tukio na watuhumiwa tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria,” alisema.

 

error: Content is protected !!