Mrema afariki dunia

HomeKimataifa

Mrema afariki dunia

Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Agustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia leo Jumapili, Agosti 21,2022 saa 12:15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31,1944 Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Msemaji wa Hospitali ya Muhimbili, Aminieli Eligasha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo.

error: Content is protected !!