Msako mifuko ya plastiki kuanza leo

HomeKimataifa

Msako mifuko ya plastiki kuanza leo

Msako wa kukamata mifuko ya plastiki katika masoko jiji la Dar es Salaam unaanza leo. Wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla alitoa agizo hilo kwa viongozi wa masoko kutekeleza agizo la Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango.

Makalla aliwaeleza viongozi hao wa masoko Dar es Salaam mwaka 2019 serikali ilizuia uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mifuko ya plastiki lakini watu wameanza tena kuitumia.

Alisema mifuko hiyo ina athari kwa mazingira, kwa afya na uchumi hivyo akaagiza ufanywe msako kukamata viwanda bubu mkoani humo. Makalla alisema mifuko hiyo inazalishwa kiholela hivyo hailipiwi kodi na walioruhusiwa kuizalisha mifuko mbadala wanafunga viwanda kutokana na kuwepo utitiri wa mifuko ya plastiki.

Aliwaagiza maofisa masoko watoe taarifa za kila siku kwa wakurugenzi kwa ajili ya kuripoti mwenendo wa mifuko hiyo. Mwenyekiti wa Soko la Tazara Veterani, Daniel Mlangu alisema amelipokea agizo hilo yuko tayari kwa ajili ya kutekeleza.

error: Content is protected !!