Lina Medina kutoka nchi ya Amerika Kusini ya Peru alivunja rekodi ya kuwa mama mchanga zaidi duniani kujifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 5, miezi 7 na siku 21. Kulingana na rekodi za hospitali, Lina alipata ujauzito akiwa chini ya umri wa miaka mitano.
Balehe uanza kwa wasichana wafikapo miaka 11 na wavulana miaka 11, lakini kisa kama cha Lina kinafahamika kama ‘precocious puberty’ ikimaanisha kuwa mtoto huanza kubalehe mapema kabla umri wa kawaida wa miaka 8 kwa wasichana na umri wa miaka 9 wa wavulana.
Mtoto huyo alipokuwa na umri wa miaka 5 na miezi 6, wazazi wake waliona kuwa Lina alikuwa na uvimbe tumboni, walimpeleka hospitali wakiwa na hofu kuwa binti yao ni mgonjwa. Daktari Gerardo Lozada alifanya uchunguzi na kugundua kuwa Lina alikuwa na ujauzito wa miezi saba. Wazazi wake hawakuamini kuwa mtoto wao alikuwa mjamzito katika umri mdogo namna hiyo. Walimtembelea mtaalamu aliyedhibitisha kuwa kweli Lina alikuwa mjamzito.
Lina alijifungua mtoto wa kiume aliyekuwa na uzani wa kilo 2.7 kupitia upasuaji. Mtoto alipewa jina Gerardo Medina. Hata hivyo hakuwahi kuweka wazi nani aliyempachika ujauzito na pengine hata yeye mwenyewe hakujua ni nani au vipi alipachikwa ujauzito.
Babake Lina Tiburelo Medina pamoja na binamu yake walizuia jela kwa muda kwa madai ya kumbaka lakini baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha waliachiwa. Kwa sasa ana umri wa miaka 87 sasa na anasemekana kuishi Peru.