Mvua kunyesha hadi mwezi Agosti

HomeKitaifa

Mvua kunyesha hadi mwezi Agosti

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema hali ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya Pwani ikiwemo jijini Dar es Salaam zitaendelea hadi mwezi ujao.

Imesema hali ya baridi kali na upepo vinatarajiwa kuendelea katika maeneo yote nchini ikiwemo Njombe, Iringa na Mbeya ambapo kiwango cha chini cha nyuzi joto kinatarajiwa kufikia 4°C.

Akizungumzia kuhusu hali ya mvua zinazonyesha, Mtaalamu wa Uchambuzi wa hali ya Hewa kutoka TMA, Rose Senyagwa amesema hali hiyo ni kutokana na hewa kunyonya unyevunyevu baharini na hivyo kusababisha mvua hizo kunyesha.

Kuhusu hali ya barafu iliyojitokeza hivi karibuni mkoani Njombe, Senyagwa amesema hali hiyo inayofahamika kama Sikitu inatokana na majimaji ya unyevunyevu kuganda na hivyo kufanya barafu hizo, hali ambayo ni kawaida kunapokuwepo na baridi kali.

 

error: Content is protected !!