Iringa, Mbeya na Njombe baridi yafika 4°C

HomeKitaifa

Iringa, Mbeya na Njombe baridi yafika 4°C

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema kwamba hali ya baridi itaendelea kuwepo ambapo katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya baridi inatarajiwa kufikia viwango vya chini vya nyuzi joto 4°C.

Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam, Mtaalam wa uchambuzi wa hali ya hewa kutoka  TMA Rose Senyagwa, amesema hali ya mvua zinazonyesha ni za nje ya msimu ambapo zimetokana na hewa kunyonya unyevunyevu baharini na hivyo kupelekea mvua hizo kunyesha.

Kuhusu hali ya barafu iliyojitokeza hivi karibuni mkoani Njombe, Senyagwa amesema hali hiyo inayofahamaika kama Sikitu inatokana na majimaji ya unyevunyevu kuganda na hivyo kupelekea barafu hizo hali ambayo ni kawaida kunapokuwepo na baridi kali.

 

error: Content is protected !!