Fahamu fukwe 5 zisizo na kiingilio Dar es Salaam

HomeKitaifa

Fahamu fukwe 5 zisizo na kiingilio Dar es Salaam

Najua utajuliza kuhusu gharama na mwingiliano wa watu ambao wakati mwingine unaweza kusababisha kukosekana kwa utulivu, usihofu zipo fukwe nyingi jijini hapa zisizo na kiingilio unazoweza kutembelea na kupata wakati mzuri wa kutafakari.

Kuhusu makelele na mwingiliano wa watu hilo usijali unachotakiwa kufanya ni kutafuta wakati mzuri wa kutembelea maeneo hayo ambao hakuna watu wengi.

“Kama unataka utulivu kwenye fukwe hii ni basi njoo asubuhi au mchana kunakuwa hakuna watu kabisa,”anasema Maulid Jamal mmiliki wa vibanda vyakutunzia nguo kwenye ufukwe wa Ununio jijini Dar es Salaam

Fukwe zilizoainishwa kwenye makala hii  zinafaa pia kwa mapumziko na shughuli nyingine za kijifurahisha ikiwemo kuogelea, kupunga upepo, mazoezi ya viungo,matembezi ya ufukweni na michezo ya watoto.

Ununio Beach 

Fukwe hii inapatikana Ununio, jijini Dar Es Salaam mita chache kutoka kituo cha daladala  cha Ununio

Sifa kuu ya fukwe hii  ni mazingira masafi kwenye maeneo mengi ya wazi yanayotumiwa kwa kupumzika, burudani na  michezo mbalimbali kama mpira na bembea kwa watoto

Eneo hilo lina migahawa yenye vyakula mbalimbali ikiwemo vyakula  vya baharini (sea foods), burudani  ya muziki kutoka kwa Dj’s au bendi zinazokuja kutumbuiza kwa ratiba walizojiwekea.

Kama unapenda huduma za ‘kishua’ yaani huduma za hadhi za juu,  kwenye fukwe huyo pia kuna hoteli jirani ambayo pia hauhitaji kiingilio ila utalazimika kununua na vinywaji kutoka hapo.

Coco Beach

Hata kama ukiwa hulijui jiji la Dar es Salaam bila shaka umesikia kuhusu Coco Beach na sifa za mazingira mazuri yaliyopo kwenye eneo hili pamoja na chakula maarufu cha  mihogo  iliyochomwa au kukaangwa kwa ustadi ambayo mara nyingi huliwa kwa mishikaki au samaki.

Hata hivyo kuna aina nyingine nyingi za vyakula unavyoweza kuvipata kwenye vibanda na migahawa iliyopo pembezoni mwa fukwe hiyo.

Fukwe hiyo ipo kilomita 1.5  kutoka kituo cha mabasi  Macho kilichopo Msasani,kutoka hapo unaweza ukapanda boda boda au bajaji ya kuchangia kwa Sh500.

Hakuna kiingilio cha kuingia kwenye fukwe hii, cha kufanya ni kutafuta tu eneo utakalo pumzika kati ya  eneo kubwa la wazi liliopo,unaweza pia kufurahia mpira wa ufukweni au kupanda farasi ambaye unatakiwa kulipia huduma hiyo ikiwa utapendelea.

Rungwe beach

Rugwe beach ni mija ya maeneo mazuri unayoweza kuyatembelea bila kiingilio, gharama pekee unaweza kukutana nazo ni za vinywaji na vyakula vinavyopatikana eneo hilo.

Fukwe hiyo inayopatikana Kunduchi, mita 1.5 kutoka kituo chamabasi cha Silver Sand ni eneo zuri la kupunga upepo, kuogelea na michezo mingine mbalimbali inayopatikana hapo.

Ukiwa ufukwenii hapo unaweza kutazama kivutio cha mawe makubwa ya baharini (matumbawe) yaliyopangwa kwa ustadi kutenganisha eneo moja na lingine lakini pia ni makazi ya viumbe wadogo wa baharini kama kaa na samaki.

Bara beach

Hii ni moja kati ya fukwe za kishua unazoweza kutembelea kabla ya mwaka 2022 haujaisha,

Fukwe hiyo iliyopo Kilomita moja kutoka kituo cha mabasi Kondo, kilichopo Ununio jijini hapa, inasifika kwa ‘location kali’ namaanisha mazingira mazuri, tulivu na yanayovutia kwa picha nzuri na matukio ya muhimu kama sikukuu za kuzaliwa na sherehe nyingine.

Licha ya kiingilio kuwa bure ni lazima mfuko wako uwe vizuri ili kukuwezesha kupata chakula na vinywaji ambavyo nilazima ununue ndani ya eneo hilo.

Pweza  Beach

Kwa wakazi wa Kigamboni na maeneo mengine jijini hapa  hii ni oja ya fukwe nzuri ya kutembelea.

Fukwe hiyo iliyopo Kigamboni  mita 10  tu kutoka barabara kuu inayoelekea Kibada, inasifika kwa usafi, safi, eneo kubwa la wazi lenye  viwanja vinavyowezesha watu kucheza  mpira wa ufukweni  (beach soka) pamoja na michezo mbalimbali ya watoto.

Kwa wanaopenda muziki na Party hapa ndio penyewe kwani kuna muziki pamoja na  bendi mbalimbali zinazokuja kutumbuiza. Kuhusu ulinzi fukwe hii imejipanga vya kutosha kuhakikisha usalama wa wakati wote mtu anapotembelea eneo hilo.

SOURCE| Nukta Habari

error: Content is protected !!