Mwamuzi Habibu Mohammed aliyechezesha pambano la Karim Mandonga na Salim Abeid amesimamishwa na Chama cha Waamuzi wa Ngumi nchini kwasababu ya kuchezesha chini ya kiwango.
Mohammed ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi wa ngumi za Kulipwa nchini ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa muda baada ya kukiri kushindwa kumudu kuchezesha pambano hilo lililopigwa usiku wa kuamkia Jumapili Septemba 25, 2022 mkoani Mtwara.
Matokeo ya pambano hilo yalifutwa na rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa baada ya mwamuzi kuonyesha kutolimudu baada ya Mandonga kupigwa na kudondoka chini lakini hakumhesabia kama kanuni zinavyotaka hadi aliponyanyuka.