Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Nyandeo, ambaye jina lake limehifadhiwa, amehukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja baada ya kupatikana na kosa la kutoa mimba.
Mwanafunzi huyo alihukumiwa kifungo cha nje kutokana na kushawishiwa kufanya kitendo hicho na mwanaume alkiempatia ujauzito huo, lakini pia ni mtoto mwenye umri wa miaka 16 na hakuisumbua mahakama wakati wa usikilizaji wa shauri hilo.
Hukumu hiyo ilitolewa Desemba 7 na Hakimu Saning’o, alisema kosa la kutoa mimba ni kinyume na kifungu cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Pamoja na hayo amemhukumu kifungo hicho kwa masharti mawili la kwanza atakuwa chini ya uangalizi wa wazazi wake na la pili atakua chini ya ofisa ustawi wa jamii na atapangiwa kwenda kuripoti kwa ofisa huyo iuli kuangalia tabia na mwenendo wake.
Katika shauri hilo washtakiwa walikua wawili , mmoja ni Winfrida Burton mkazi wa Chikago A, wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro alimuuzia mwanafunzi huyo vidonge visivyojulikana huku akijua ni mjamzito.
Mshtakiwa wa pili alikua mwanafunzi mwenyewe kwa kosa la kumeza dawa na kutoa mimba.