Mwenge watembelea miradi ya elimu na nishati Tunduru

HomeKitaifa

Mwenge watembelea miradi ya elimu na nishati Tunduru

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, umetembelea mradi wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Tunduru, unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 24. Mradi huu unalenga kuboresha mazingira ya kupikia kwa wanafunzi huku ukihimiza matumizi ya nishati salama kwa afya na rafiki kwa mazingira.

Matumizi haya ya nishati safi yanaunga mkono na kwenda sambamba na ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ya kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, kwa lengo la kulinda afya ya binadamu na kuhifadhi mazingira.

Aidha, Mwenge huo pia umepitia mradi wa ujenzi wa mabweni mawili pamoja na matundu sita ya vyoo katika shule hiyo, ukiangazia juhudi za kuboresha mazingira ya elimu, afya, na ustawi wa wanafunzi.

Miradi hiyo inalenga kuinua kiwango cha elimu, afya na maendeleo endelevu kwa kutumia teknolojia jumuishi na rafiki kwa mazingira.

error: Content is protected !!