Mwijaku: Diamond na Harmonize wamerekebishana

HomeBurudani

Mwijaku: Diamond na Harmonize wamerekebishana

Mtangazaji wa kipindi cha Leo tena kinachorushwa kwenye redio ya Clouds Fm, Mwijaku ameeleza kuhusu sakata linalowahusu wasanii wakubwa wawili kutoka Tanzania, Harmonize na Diamond Platnumz kwamba maneno yanayoendelea kwenye mitandao sio bifu bali wameamua kuelekezana namna ya kuishi.

Ameongea hayo baada ya kuulizwa kuhusu maneno aliyoandika Diamond Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba vijana wajifunze kuwa na heshima na nidhamu na pia kuacha matumizi ya mihadarati huku ikisemekana kwamba ujumbe huo unamlenga nyota wa zamani wa kundi la Wasafi, Harmonize na baada ya maneno hayo Mmiliki huyo wa lebo ya Konde Boy na yeye aliandika kwamba watu waache matumizi ya ‘ngada’ (dawa za kulevya).

“Mwenzio akikosea unamwambia, mmoja kamwambia bwana acha mihadarati na yeye akamwambia acha kula unga, kwa hiyo tayari tunarekebishana,” alisema Mwijaku.

Mwijaku akiongea kuhusu ushahidi kama wasanii hao wanatumia vilevyi hivyo, amesema kwamba vitu vingine sio lazima ushahidi kwani kwa mwonekano tu mtu unaweza kumuona. Pi aliwataka wasanii waache matumizi ya vilevi hivyo kwani baadhi ya makampuni makubwa na taasisi zitawakimbia kwani hawawezi kufanya kazi na mtu anayetumia mihadarati na kula ‘unga’.

error: Content is protected !!