Mafuta ni bidhaa muhimu duniani inayotumika katika kuzalisha nishati viwandani, kwenye vyombo vya usafiri na sehemu nyingine zenye mitambo mbalimbali.
Zipo nchi ambazo zinazalisha na kuhifadhi sehemu kubwa ya mafuta yanayotumika duniani kote.
Zifuatazo ni nchi zenye hifadhi kubwa zaidi ya mafuta duniani (takwimu za mwaka 2021)
1. Venezuela
Venezuela wana zaidi ya mapipa bilioni 300 ya mafuta, hifadhi ambayo ni kubwa kuliko hifadhi ya mafuta katika nchi nyingine yoyote duniani.
2. Saudi Arabia
Nchi hii iliyopo katika bara la Asia, lina mapipa ya mafuta zaidi ya bilioni 266.
3. Canada
Taifa hilo lililopo katika bara la Amerika, linamiliki zaidi ya mapipa ya mafuta bilioni 169 yakichimbwa zaidi kwenye jimbo la Alberta.
4. Iran
Licha ya kukumbwa na vikwazo vya kiuchumi kutoka kwa Marekani na mataifa mengine mara kwa mara, Iran haijawahi kuacha shughuli zake za uchimbaji wa mafuta.
Iran inamiliki mafuta ya mapipa zaidi ya bilioni 158.
5. Iraq
Miji ya Basra, Baghdad na Ramadi ina kiwango kikubwa cha mafuta, na hivyo kuifanya Iraq iwe na mapipa zaidi ya bilioni 142.
6. Kuwait
Kuwait ina mapipa ya mafuta tarkiban bilioni 101.
7. Falme za Kiarabu (United Arab Emirates)
Falme saba za kiarabu (Abu Dhabi, Ajman, Dubai, Fujairah, Ras Al Khaimah, Sharjah na Umm Al Quwain) kwa pamoja zina mapipa ya mafuta zaidi bilioni 97.
8. Urusi
Urusi ina mapipa ya mafuta zaidi ya bilioni 80.
9. Libya
Libya ina mapipa ya mafuta zaidi ya bilioni 48.
10. Nigeria
Nchi hii ya Afrika ina mapipa ya mafuta zaidi ya bilioni 37
Chanzo cha takwimu hizi ni mtandao wa ‘World Population Review’