Nchi 20 kushiriki maonesho ya Sabasaba

HomeKitaifa

Nchi 20 kushiriki maonesho ya Sabasaba

Maandalizi ya Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Sabasaba yamekamilika kwa asilimia 95, na nchi 20 ikiwemo Marekani zimethibitisha kushiriki maonesho hayo.

“Kwa kiasi kikubwa mabanda yote na maeneo ya wazi yameshapata washiriki, ambapo wapangaji wa kudumu wote watashiriki na wapangaji wa msimu nao wamekwisha oneshwa maeneo yao, kilichobaki nikulipia,” alisema Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), David Langa.

Amesema maonesho hayo yatafunguliwa Juni 28, na yataendelea hadi July 17, mwaka huu.

Baadhi ya nchi ambazo zimethibitisha kushiriki ni Botswana, China, India, Ujerumani, Syria, Iran, Kenya, Poland, Morocco, Rwanda, Nigeria, Ghana, Misri, Uganda, Burundi, Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Marekani inashiriki kwa mara ya kwanza tangu maonesho hayo yaanze miaka 46 iliyopita.

 

error: Content is protected !!