“Lord Bless Africa” yani “Mungu ibariki Afrika” ni wimbo ulioandikwa na Enoch Sontonga, mchungaji wa Xhosa nchini Afrika Kusini mwaka 1897 ambapo yeye aliupa jina la “Nkosi sikelei Afrika” na baadae ukaanza kutumika kwenye nchi zingine 5 barani Afrika nazo ni Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia.
Afrika Kusini
Wimbo huu ulianza kutumika Afrika Kusini mwaka 1897 baada ya mfumo wa kitaasisi wa ubaguzi wa rangi “Apartheid” uliokuwepo Afrika Kusini na Magharibi (Namibia) kuanzia mwaka 1948 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990. Wimbo huu huimbwa kwa lugha 5 nazo ni Xhosha, Zulu, Sesotho, Afrikana na Kiingereza.
Tanzania
Kwa Tanzania wimbo huu unajulikana kama “Mungu Ibariki Afrika” Ulianza kutumika nchini mwaka 1961 baada ya uhuru na bado unatumika mpaka sasa. Wimbo huu huimbwa mashuleni kila siku asubuhi kama njia moja wapo yakusambaza uzalendo kwa nchi.
Zambia
Zambia walianza kutumia ukiwa na jina la “Nkosi Sikelei Afrika” kuanzia mwaka 1964 mpaka 1973 na baadae mashahiri yalibadilishwa na kuwa “Stand and Sing of Zambia, Proud and Free” na ndio wanatumia mpaka sasa kama wimbo wa Taifa.
Hata hivyo Zimbabwe na Namibia walibadirisha wimbo huyo na sasa kila nchi inawimbo wake wa taifa tofauti kabisa na Nkosi Sikelei Afrika kutokana na sababu zifuatazo:
Zimbabwe
Uianza kutumika mwaka 1980 na mwaka 1994 ulibadilishwa na kuwa “Blessed be the land of Zimbabwe” na pia wanautumia kwenye shughuli rasmi za nchi yao kama ilivyo kwenye mataifa mengine.
Namibia
Ulitumika kwenye uhuru wa nchi hii mwaka 1990 na baadae ulibadilishwa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa Namibia ambapo shindano liliandaliwa kutafuta mtu atakaye andika wimbo mpya na Axali Doeb akaibuka mshindi kwakuandika wimbo “Namibia Land of Brave” na mwaka 1991 ukaanza kutumika rasmi kama wimbo wa taifa.
Hivyo mpaka sasa, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia bado wanatumia wimbo huu wa “Nkosi sikelei Afrika” uliandikwa na Enoch Sontoga, ukitaka kugundua pata muda zisikiliza nyimbo hizi za haya mataifa matatu.