Kwa mujibu wa tathmini ya Benki ya Dunia, Zimbabwe ndiyo nchi inayoongoza kuwa na gharama kubwa ya chakula huku ikitajwa kuongezeka kwa asilimia 321 katika kipindi cha mwaka mmoja kwa mujibu wa tathmini ya Benki ya Dunia (WB).
Katika tathmini hiyo, nchi zingine ambazo zimeonesha kuwa na mfumko wa bei za vyakula ni pamoja na Lebanon (208%), Venezuela (158%), Turkiye (99%), Argentina (87%), Sri Lanka (86%), Iran (84%), Rwanda (41%), Suriname (40%) na Lao PDR (39%).