Shirika la Ndege Tanzania(ATCL) limesema inatarajia kupokea Ndege nne kwa mwaka huu ambapo ndege kubwa ya mizigo itawasili nchini mwishoni mwa mwezi Machi na kuanza kutumika mwezi Aprili.
Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ndege nyingine itawasili mwezi Agosti huku zingine mbili zikiwasili mwishoni mwa mwaka huu.
“Serikali ilisema inanunua ndege mpya kuongeza uwezo wa Air Tanzania kutoa huduma na mpaka sasa ndege nne ziko katika hatua za mwisho na ndege ya kwanza ni ya mizigo 767 ina ujazo wa tani 54 .
Matindi amesema kunamahitaji makubwa sana katika masoko kama China, India, Mashariki ya Kati hivyo serikali imeona kuna umuhimu kuhakikisha bidhaa zetu zinafika kwenye soko kwa wakati ili kushindana.