NHC yawashukia wadaiwa sugu

HomeKitaifa

NHC yawashukia wadaiwa sugu

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kuanza kuwaondoa wapangaji wa nyumba zake ambao ni wadaiwa sugu huku kwa mujibu wa Naibu Waziri wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amesema shirika hilo linadai wapangaji takribani shilingi bilioni 26.

Madai hayo yamechangia uzoroteshaji kasi ya utendaji kazi wa shughuli za kila siku za shirika ikiwemo ukarabati wa nyumba hizo.

“Tutakachofanya sasa, yoyote aliyelikimbikiza deni na tumeshampa notisi lakini bado halipi kodi basi zoezi la kumuondoa litafanyika bila hata kumtaarifu upya,” amesema Dkt Mabula.

Dk Mabula amesema operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu inahusisha pia kuwaondoa wapangaji wote ambao sio waaminifu, anasema kuna wapangaji walipangishwa na shirika nyumba kwa bei rahisi lakini wao wamepangisha kwa watu wengine kwa bei ya juu zaidi.

Aidha pia shirika hilo limeanza kufanya marekebisho katika nyumba zake ikiwa ni mpango wake wa miaka mitano huku tayari shilingi bilioni 50 zikiwa zimetengwa.

error: Content is protected !!