Njia 6 za kukabiliana na majanga ya moto

HomeElimu

Njia 6 za kukabiliana na majanga ya moto

Hivi karibuni kumekuwa na majanga mengi ya moto ambayo husababisha uharibifu wa mali na kugharimu maisha ya watu, kutokana na miundombinu duni ya majengo majanga ya moto yameendelea kuwakumba watu wengi hata hivyo zipo njia kadha unazoweza kutumia kukabiliana na tatizo hili;

1. Tumia soketi na swichi vyema
Kutokana na ujenzi duni, si jambo la kustajabisha kukuta nyumba moja ina soketi moja au mbili. Hili husababisha watu kujaza kila kifaa kwenye soketi hiyo moja, swala ambalo hufanya soketi hiyo izidiwe na kuwaka moto. Pia hakikisha watoto hawachezei soketi au swichi za umeme.

2. Tumia mfumo bora na salama wa umeme
Majanga mengi ya moto husababishwa na hitilafu zinazotokana na mifumo duni ya umeme. Tumia mtaalamu, yaani fundi anayefahamu vyema taaluma ya umeme. Ukimtumia mtu asiye na ujuzi wa kutosha atakuwekea mfumo duni unaoweza kusababisha moto.

3. Tumia jiko vyema
Ikiwa una jiko lililoko ndani ya nyumba unatakiwa kuchukua tahadhari zaidi. Haijalishi ni jiko la umeme, gesi au mafuta unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo ili kuepuka majanga ya moto. Usiache watoto wachezee jiko au kutumia jiko bila uangalizi, epuka kutumia jiko la mkaa ndani ya nyumba kwani ni moja wapo chanzo cha majanga ya moto.

4. Usiache moto ukiwaka karibu na nyumba
Kuwasha moto karibu na nyumba kuna hitaji tahadhari kubwa sana kwani unaweza kusababisha majanga ya moto sababu ya upepo unaopuliza hivyo inabidi uwe makini sana.

5. Andaa miundombinu na vikabili moto
Weka vifaa vya kuhisi moto au moshi (smoke detectors). Hakikisha watu wanaweza kujiokoa kwa kupitia madirishani au kwenye milango ikiwa moto utatokea. Yani jenga madirisha na milango inaruhusu watu kujiokoa. Weka vifaa vya kuzimia moto kama vile mpira wa maji wa kuzimia moto pamoja na mitungi ya hewa.

error: Content is protected !!