Njia wanazotumia trafiki kupokea rushwa barabarani

HomeKitaifa

Njia wanazotumia trafiki kupokea rushwa barabarani

Rushwa ni miongoni mwa mambo yanayopigwa vita kutokana na kurudisha nyuma maendeleo katika sekta na taasisi mbalimbali za umma hasa ya Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani.

Hivi karibuni vitendo vya rushwa vimeshamiri kwenye baadhi ya mikoa baada ya kuripotiwa kwa matukio mbalimbali kutoka kwa askari wa kikosi hicho.

Zifuatazo ni njia wanazotumia askari hao wakati wakupokea rushwa.

LESENI

Baadhi ya madereva wameeleza kwamba baada ya askari kukusimamisha anakuambia unakosa fulani hivyo nipe kiasi fulani la si hivyo anakuandikia cheti. Kwa hiyo wakati unampa fedha anataka umkunjie kwa chini ukiwa unampa leseni hali ambayo mtu wa pembeni hawezi kutambua kitu gani kinaendelea.

RISITI

Askari anapokukamata humtaka dereva au kondakta kuikunja fedha ndani ya risiti na kumpatia wakati huo wakiwa wamesimama nyuma ya gari mahali ambapo mtu sio rahisi kuwaona.

KOFIA/VICHWA NDANI YA GARI

Askari wengine huhitaji wawekewe fedha ndani ya kofia zao, au anapoingiza kichwa ndani ya gari anakuonyesha ishara kuwa udumbukize ndani ya kufia yake, kitendo ambacho ni ngumu mtu anayepita pembeni kutambua kwani atahisi kuwa kuna mazungumzo yanaendelea.

VIBANDA

Baada ya askari kukamata gari humtaka dereva aende kuweka fedha kwenye kibanda ambacho kipo karibu na eneo husika ili wasimuandikie cheti kulingana na kosa analokutwa nalo.

MAWAKALA

Wengine hutumia watu tofauti na wao kupokea fedha kutoka kwa madereva na watu hao wanakuwa wanasimama au wanaendesha biashara karibu na mazingira wanapolikamatia gari.

LESO

Baadhi ya askari wa usalama barabarani hupokea rushwa kwa kutumia tissue na leso, fedha huviringishwa kwenye leso na askari hupokea.

Hata hivyo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa amewataka askari wa usalama barabarani kutokwenda na magari kwenye sehemu zao za kazi akidai kuwa magari hayo yanatumika kupatania rushwa na kueleza kuwa kitendo hiko kinatengeza taswira mbaya ya Jeshi hilo.

error: Content is protected !!