Mapato ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yameongezeka mara mbili kutokana na ofa iliyotolewa na Rais Samia Suluhu kwa wananchi ya kulipa kodi bila faini.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masame alisema tangu kutolewa kwa ofa hiyo mapato ya kodi ya pango yameongeza kutoka wastani wa kati ya sh bilioni 8 na sh bilioni 10 kwa mwezi hadi wastani wa sh bilioni 15 kila mwezi.
Masame alisema pia mwitikio wa kulipa kodi ya pango la ardhi nao umeongezeka kutoka asilimia 40 hadi asilimia 60 kati ya wamiliki ardhi zaidi ya milioni 2.
Aidha, Masame alisema kabla ya ofa iliyotolewa na Rais Samia, wizara ilikuwa na mashauri 3,4000 ya watu waliokuwa na malimbikizo ya madeni na kwamba asilimia 90 ya hao walilipa baada ya kufikishwa mahakamani.