Tanzania na Oman zimeweka mikakati ya ushirikiano katika sekta ya maasiliano, habari na teknolojia.
Mikakati hiyo iliwekwa juzi wakati Waziri wa Habari, Nape Nnauye alipokutana na Waziri wa Habari wa Oman, Dk Abdullah bin Nasser bi Khalifa Al-Harassi nchini Oman.
Miongoni mwa mikakati hiyo ni nchi hizo kuweza kutumia vyombo vya habari kuhabarisha umma kuhusu masuala ya kijamii, kutangaza tamaduni na kubadilishana ujuzi wa teknolojia.
Nape alisema kutokana na uhusiano wa kihistoria ya muda mrefu kati ya Tanzania na Oman, nchi hizo zinapaswa kuhabarishwa ipasavyo kuhusu undugu wa damu kati ya watu wa Oman na Watanzania ili kuendela kutunza uhusiano huo.
Walikubaliana kuwa Oman kupitia vyombo vyake vya habari itaitangaza Tanzania katika mataifa mengine ili kuvutia biashara, uwekezaji na utalii.