Penzi la Rayvanny na Paula kaa la moto

HomeBurudani

Penzi la Rayvanny na Paula kaa la moto

Penzi la muimbaji kutoka lebo ya WCB maarufu kama Rayvanny pamoja na mtoto wa muigizaji Kajala anaejulikana kama Paula limeingia sintofahamu baada ya wawili hao kila mmoja kumu “unfollow” mwenzie katika mtandao wa Instagram.

Paula kwasasa yuko nchini Uturuki kwaajili ya masomo lakini huku nyumbani Tanzania kumekua na matukio mengi yanayomuhusisha Rayvanny pamoja na mzazi mwenzie Fahma, kikubwa zaidi siku moja kabla ya wawili hao kila mmoja kuacha kumfollw mwenzie Fahyma aliweka wimbo mpya wa Rayvanny alioimba na msanii Maluma unaoitwa Mama Tetema.

Fahyma alipost Katika Insta Story yake na kuandika “super proud of you”, nje na kuweka wimbo huo katika Insta story yake wawili hawa wamekua wakidaiwa kuwa pamoja mara nyingi huku Fahyma akikataa kuwa sio kweli.

Ikumbukwe kuwa Fahyma alisema kuwa yeye hawezi kuachwa na Rayvanny lakini hata baada ya kuachana na Rayvanny kuanza mahusiano na Paula, Bado Fahyma alisikika akisema bado wanapendana bado haijafahamika kama wawili hawa wamerudiana na kama Rayvanny na Paula wameacha au bado wako pamoja.

error: Content is protected !!