Wapenzi wafunga ndoa ‘Zoom’

HomeKimataifa

Wapenzi wafunga ndoa ‘Zoom’

Mwanadada Brit Ayse kutokea Lancaster Marekani mwenye umri wa miaka 26 amefunga ndoa na mpenzi wake Darrin mwenye umri wa miaka 24 kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kwa njia ya video, Brit na Darrin walikutana mtandaoni kipindi cha ugonjwa wa Uviko 19.

Brit anasema alijiunga na kikudi cha kutafuta marafiki kwenye mtandao wa Facebook lakini baade akajikuta ameanza kumpenda Darren, Anasema Novemba mwaka jana walianza kuwasiliana na kupigiana kwa njia ya video hali iliyopelekea kuzoeana na kujihisi wapo karibu zaidi hadi Brit kuamua kutengeneza mdori unaefanana na Darren ili awe anamuona muda wote.

Kutokana na kuwepo kwa zuio la kutotoka ndani Darren na Bryte walishindwa kukutana ila baadae Darren aliongea na baba wa Brit na kumuomba ruhusa ya kumvisha pete binti yake, Brit anasema siku ya tukio Darren alimpigia simu akiwa mwenye furaha sana kuliko kawaida na akapiga goti ishara ya kumuomba akubali kuolewa na yeye Brit alikubali.

Pamoja na kwamba wamefunga ndoa lakini bado wawili hao hawajawahi kukutana mpaka sasa, wawili hao wanatarijia kusherekea pamoja baada ya kuondolewa kwa zuio la kukaa ndani.

error: Content is protected !!