Harmonize amfichua mrithi wa Kajala

HomeBurudani

Harmonize amfichua mrithi wa Kajala

Mwimbaji na mmiliki wa rekodi lebo ya Konde Gang Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka video kwenye insta story ambapo ilisikika sauti yake na mwanadada wakiwa wenye furaha huku vicheko na sauti za mahaba zikitawala.

Katika video hiyo kuna picha inaonesha mkono wa mwanadada akiwa ameshika picha inayoonyesha harmonize akiwa amemkumbatia kwa nyuma msichana mwenye asili ya kizungu huku chini ikandikwa “what a memory”, yaani ni kumbukumbu ambayo harmonize hawezi kuisahau.

Harmonize na Kajala waliachana huku sababu ikiwa ni Harmonize baada ya vilipovuja picha na video zilizodaiwa ni za harmonize akidai penzi kwa Paula. Harmonize kabla ya kuwa wa Kajala aliwahi kuwa na mwanamitindo Sarah mwenye asili ya kitaliano.

 

error: Content is protected !!