Rais akimbia na mabegi ya fedha

HomeKimataifa

Rais akimbia na mabegi ya fedha

Piraz Ata Sharifi  aliekuwa mlinzi wa Rais wa Afghanistan amesema baada ya serikali ya nchi hiyo kupinduliwa, aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Ashraf Ghan alikimbia akiwa na mabegi yenye fedha ambazo zinakaridiwa kuwa ni mabilioni ya dola za kimarekani.

Piraz amesema anauthibitisho wa video unaomuonesha mtu ambaye alienda kutoa fedha hizo benki na kuzipeleka kwa Rais huyo kisha Rais na familia yake wakaondoka kuelekea nchini Qatar.

Utawala wa Ashraf Ghani uliangushwa Agosti mwaka huu na kundi la Taliban ambalo ndilo linaongoza dola ya Afghanistan kwa sasa.

error: Content is protected !!