Rais Samia aanza ziara ya siku saba nchini Korea

HomeKimataifa

Rais Samia aanza ziara ya siku saba nchini Korea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya siku saba katika Jamhuri ya Korea Kusini na leo anatarajiwa kukutana na wadau na wataarishaji wa filamu nchini humo.

Katika ziara hiyo, Rais Samia atashuhudia utiaji saini wa kadhaa ikiwamo wa mkopo nafuu wa dola bilioni 2.5 sawa na shilingi trilioni 6.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya afya, elimu, miundombinu pamoja na mikataba ya uchumi wa buluu, madini, kilimo, sanaa na utamaduni.

Rais Samia ambaye yupo kwenye ziara hiyo ya kikazi kwa mwaliko wa mwenyeji wake Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini, ameambata na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya.

Pia, Rais Samia atatunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa na Chuo Kikuu cha Anga cha Korea Kusini kwa kutambua mchango wake katika sekta hiyo.

error: Content is protected !!